Adele amempa Beyonce tuzo yake ya Grammy?

Adele tuzo za Grammy Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Adele ameshinda jumla ya tuzo nne za Grammy

Nyota wa muziki wa Adele anaonekana kukataa tuzo ya Grammy aliyotunukiwa kwa kuwa na albamu bora zaidi.

Badala yake, amesema Beyonce ndiye aliyestahiki zaidi kutunukiwa tuzo hiyo.

Adele alipewa tuzo hiyo kwa albamu yake kwa jina 25 ambayo imevuma sana duniani, lakini ameambia waliohudhuria kwamba, "Haiwezekani kwangu kupokea tuzo hii".

"Ni heshima kubwa sana kwangu na nashukuru, lakini Beyonce ndiye mwanamuziki bora maishani mwangu".

Ushindi wa Adele dhidi ya Beyonce bila shaka utachocheza zaidi malalamiko kwamba tuzo za Grammy sana huwabagua wasanii weusi.

Wasanii kadha wakiwemo Frank Ocean na Kanye West, waliamua kususia sherehe za mwaka huu za kutoa tuzo kwa washindi kwa msingi huo.

Ocean hata alikataa kuwasilisha albamu yake maarufu ya Blonde ishindanie tuzo akisema tuzo za Grammy hazionekani "kuwakilisha vyema watu wa eneo ambalo nimetoka mimi, na kudunisha watu ambao ninadunisha".

Miaka miwili iliyopita, West aliondoka kwa hasira jukwaani baada ya Beyonce kukosa kutangazwa mshindi kwa albamu yake kwa jina Beck's Morning Phase.

Hata hivyo, albamu ya Adele ya 25 bila shaka ndiyo iliyouza nakala nyingi zaidi miongoni mwa zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo. Iliishinda albamu ya Lemonade yake Beyonce kwa 10 kwa 1.

Haijabainika iwapo Adele ataikataa rasmi tuzo hiyo.

Haki miliki ya picha AP

Iwapo atafanya hivyo, basi itakuwa ni mara ya pili pekee kwa jambo kama hilo kutokea.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1990, pale Sinead O'Connor alipoikataa tuzo ya albamu bora mbadala kwa albamu yake I Do Not Want What I Have Not Got, na kudai sherehe hizo zilikuwa zimeingiliwa sana na "biashara".

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Beyonce akitumbuiza
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Beyonce alitangaza majuzi kwamba anatarajia kujifungua pacha

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii