Uhusiano kati ya afisa wa White House na Urusi, wazua utata Marekani

Michael Flynn alikana kuzungumzia vikwazo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michael Flynn alikana kuzungumzia vikwazo

Afisa wa cheo cha juu kwenye Ikulu ya Marekani amemtetea mshauri wa ngazi ya juu wa masuala ya ulinzi Michael Flynn, kufuatia utata unaohusu uhusiano na Urusi.

Bwana Flynn anaripotiwa kuzungumzia vikwazo na balozi wa Urusi Sergei Kislyak wiki kadha kabla ya kuapishwa kwa Trump.

Utata huo unaibuka wakati Trump, anakabiliwa na changamoto za usalama wa kitaifa kufuatia hatua ya Korea Kaskazini kulifanyia jaribio kombora siku ya Jumapili.

Bwana Flynn huenda akahusika kuamua hatua ya Marekania kujibu jaribio hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisa wa cheo cha juu wa White House alikataakumuunga mkono Flynn

Bwana Flynn anajulikana kwa kufanya mazungumzo na bwana Kislyakl mara kadha kwa njia ya simu mwezi Disemba.

Bwana Flynn na Makamu wa Rais Mike Pence, wote walikana kuwa wawili hao walizungumzia vikwazo vya Marekani, ilivyoiwekea Urusi kufuatia vitendo vyake nchini Ukrain na kudukuliwa kwa chama cha Democratic nchini Marekani.

Stephen Miller, ambaye ni mshauri mkuu wa masuala ya sera wa Trump, alikataa kusema lolote wakati wa mahojiano ikiwa Trump anamuunga mkono Flynn.

Alipoulizwa ikiwa Rais bado ana imani na bwana Flynn, bwana Miller alisema kuwa hilo ni swali kwa Rais. Maafisa wengine wa Ikulu nao walikataa kuzungumzia suala hilo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bwana Flynn alipigwa picha akipata chakula na Rais wa Urusi Vladimir Putin mwezi Disemba 2015