Playboy kuchapisha tena picha za utupu

Playboy Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Jarida hilo limepakia jalada la makala ya Machi-Aprili kwenye Twitter

Jarida la Playboy limetangaza kwamba litaanza kuchapisha tena picha za utupu, na kubatilisha uamuzi wa awali uliotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

Hatua ya sasa imetangazwa na afisa mkuu mpya wa ubunifu katika jarida hilo Cooper Hefner, ambaye amesema uamuzi wa kuondoa kabisa picha za utupu "lilikuwa kosa".

"Leo tunarejesha utambulisho wetu na kutwaa tena sifa zetu," aliandika kwenye Twitter.

Jarida hilo linalochapishiwa Marekani pia limepakia mtandaoni jalada la makala yake ya Machi-Aprili ya jarida hilo na kutumia kitambulisha mada #NakedIsNormal (Utupu ni kawaida).

Baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wamefurahia uamuzi huo, lakini wengine wamesema uamuzi huo umechukuliwa "kwa sababu majarida hayo hayanunuliwi sana. Bahati mbaya kwamba siku hizi picha na video za utupu zinapatikana kwa urahisi sana bila malipo."

Jumatatu, bw Hefner aliandika: "Nitakuwa wa kwanza kukiri kwamba njia ambayo jarida hili lilitumia kuonesha utupu ilipitwa na wakati.

"Utupu haujawahi kuwa tatizo kwa sababu utupu si tatizo," Hefner, 25, ambaye ni mwana wa kiume wa mwanzilishi wa Playboy Hugh Hefner alisema.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Playboy ilianzishwa na Hugh Hefner mwaka 1953

Samir Husni, profesa wa uanahabari katika chuo kikuu cha Mississippi anasema marufuku ya utupu iliyotolewa na Playboy awali huenda iliwapoteza wasomaji wengi kuliko wale iliyowavutia.

"Playboy na wazo la kutokuwa na utupu hayaendani kwa pamoja," aliambia Associated Press.

Jarida hilo hata hivyo bado lina kibarua kigumu kuwavutia vijana enzi hizi za dijitali ambapo picha na video za utupu zinapatikana kwa urahisi mtandaoni, Bw Husni alisema.

Idadi ya nakala za jarida la Playboy zinazonunuliwa ilishuka kutoka 5.6 milioni miaka ya 1970 hadi 800,000 kufikia mwaka 2016.

Mada zinazohusiana