Watoto na watu wazee ndio walichangia zaidi kusambaa kwa Ebola

Watoto na watu wazima ndio walichangia zaidi kusambaa kwa Ebola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watoto na watu wazima ndio walichangia zaidi kusambaa kwa Ebola

Visa vingi vya mlipuko mkubwa zaidi duniani wa ugonjwa wa Ebola vilisababishwa na wagonjwa wachache, kufuatia utafiti uliofanywa.

Takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 61 ya visa vya ugonjwa wa bola vilisababishwa na asilimia 3 ya watu waliaokuwa wameambukizwa.

Watoto na watu wazee ndio huenda walichangia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 28,600 waliambukizwa ugonjwa wa Ebola, wakati wa mlipuko wa mwaka 2014 na 2015 magharibi mwa Afrika ambapo karibu watu 11,300 waliaga dunia.

Ebola ilisambaa kwa njia gani?

Utafiti huo ulifanywa ndani na nje ya mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.

Kwa kufuatilia jinsi ugonjwa huo ulivyosambaa, watafiti waligundua ni watu wangapi kila mtu kila mtu aliyekuwa na virusi hiyo aliambukiza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watoto na watu wazima ndio walichangia zaidi kusambaa kwa Ebola

Watoto walio chini ya miaka 15 na watu wazima walio na zaidi ya miaka 45, ndio walichangia zaidi na kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.

Waambukizaji sawa na hawa, wamehusika na kuchangia maambukizi ya magonjwa kama wa (Sars) pamoja na homa ya mashariki ya kati (Mers).