Watu 7 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wahukumiwa kifo Somalia

Watu 7 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wahukumiwa kifo Somalia
Image caption Watu 7 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wahukumiwa kifo Somalia

Mahakama moja ya kijeshi eneo lililojitenga nchini Somalia la Puntland, imewahukumu washukiwa saba wa ugaidi kifo kwa kuwaua maafisa kadha wa vyeo vya juu wa eneo hilo, akiwemo mkurugenzi wa ikulu ya rais wa Puntland Aden Hurus.

Baadhi ya wanaume hao wanalaumiwa kwa kuwa wanachama wa mrengo wa al-Qaaeda wa kundi la al-Shabab, waliongea kwa sauti wakisema kuwa hawana hatia kabla ya kusomwa kwa hukumu na mahakama ya mji wa Basaso.

Wakili wao alisema atakata rufaa kupinga hukumu hiyo kwa sababa hakuna ushahidi wa kutosha kuwahukumu watu hao saba.