Bwawa la Ethiopia lasababisha upungufu wa maji Kenya

Picha za satelite za Gibe III na za Ziwa Turkana. Haki miliki ya picha Human Rights Watch
Image caption Picha za satelite za Gibe III na za Ziwa Turkana.

Bwawa kubwa lililojengwa nchini Ethiopia limesababisha upungufu mkubwa wa maji kwenye ziwa Turkana kaskanzi mwa Kenya.

Hali hiyo pia imetishia maisha ya takriban watu 500,000 ndani ya nchi hizo mbili kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch.

Human Rights Watch ilitoa picha za satellite zinazoonyesha kuongezeka kwa maji karibu na bwawa na kupungua kwa katika kingo za ziwa Turkana.

Bwawa la Gibe III pamoja na mashamba makubwa ya miwa yamesababisha kushuka kwa kiwango cha maji ya ziwa Turkana kwa mita 1.5 kutoka viwango vya awali.

Katika sehemu nyingi picha hizo zinaonyeha maji yakiwa yamepungua umbali wa kimomita 1.7.