Je nani ni muuaji wa Kim Jong Nam?

Korea ya Kaskazini
Image caption Kim Jong Nam, marehemu kwa sasa

Aliyekuwa ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, inaarifiwa kuwa chanzo cha kifo chake ni mauaji dhahiri yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Nao polisi nchini Malysia wamesema kwamba Kim Jong Nam alishambuliwa siku ya Jumatatu wakati alipokuwa akitarajia kuabiri kuelekea Macao.

Kabla hajafariki dunia wakati akipelekwa hospitalini, alitoa maelezo kuwa alivutwa kutoka kwa nyuma na kumwagiwa kitu kioevu usoni mwake.

Uchunguzi wa kitabibu utafanywa ili kuweza kubaini chanzo cha kifo, huku kukiwa na tetesi kuwa huenda kimiminika alichomwagiwa usoni huenda ikawa ni sumu.

Chanzo kutoka katika serikali ya Marekani kinasema kwamba wanaamini kwa dhati kuwa Bw Kim, aliyekuwa anaishi uhamishoni, aliuawa na mawakala kutoka Korea Kaskazini.

Mwaka 2001 Kim alikamatwa akijaribu kuingia Japan akitumua pasipoti bandia.

Aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kuzuru eneo la burudani la Disneyland mjini Tokyo.

Kim alikwa akionekana kama mtu ambaye angemrithi babake lakini kitendo hicho kilisababisha wao kutofautiana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kim Jong-nam alitumia muda wake mwingi nje ya Korea Kaskazini

Kim Jong-nam ndiye mtoto wa kwanza wa kiume wa Kim Jong-il, ambaye aliitawala Korea Kaskazini kuanzia mwaka 1994 hadi wakati wa kifo chake mwaka 2011.

Baada ya nduguye mdogo wa kambo kuchukua uongozi wa Korea Kaskazini wakati babake alifariki mwaka 2011, Kim Jong-nam hakuoneka saana na alitumia muda wake mwingi nje ya nchi hasa Macau , Singapore na China.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii