Kifo cha Kim Jong-nam: Mwanamke akamatwa Malaysia

Polisi Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur Februari 15, 201 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi nchini Malaysia wanawasaka washukiwa wengine

Polisi nchini Malaysia wamemkamata mwanamke mmoja kuhusiana na mauaji ya nduguye wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Polisi wanasema mwanamke huyo amekamatwa katika uwanja wa ndege uliopo katika mji mkuu Kuala Lumpur ambapo Kim Jong-nam alishambuliwa.

Baadhi ya taarifa zinasema huenda alipewa sumu.

Mwanamke aliyekamatwa alikuwa na hati ya kusafiria ya Vietnam.

Polisi nchini Malaysia wamesema bado wanawatafuta washukiwa wengine "kadha).

Mwanamke huyo alikamatwa mwendo wa saa mbili unusu asubuhi Jumatano saa za Malaysia.

Mshukiwa huyo alitambuliwa kwa kutumia video za kamera za siri, CCTV, katika uwanja wa ndege na alikuwa peke yake wakati wa kukamatwa kwake.

Ametambuliwa kama Doan Thi Huong, aliyezaliwa 31 Mei 1988, kwa mujibu wa pasipoti aliyokuwa nayo.

Picha za CCTV ambazo zinasambazwa kwenye vyombo vya habari zinawaangazia wanawake wawili ambao walikuwa wameambatana na Bw Kim, na ambao muda mfupi baadaye walionekana wakiondoka eneo hilo kwa kutumia teksi.

Picha iliyopeperushwa na vyombo vya habari Korea Kusini na Malaysia ilimwonesha mwanamke, anayedaiwa kuwa mmoja wa washukiwa, akiwa na fulana iliyokuwa imeandikwa "LOL" upande wa mbele.

Haki miliki ya picha AFP

Maafisa wa Korea Kaskazini wazuru hospitali

Awali, shirika la habari la serikali ya Malaysia Bernama liliripoti kwamba mwanamke kutoka Myanmar alikamatwa na kuzuiliwa uwanja wa ndege.

Haijabainika iwapo taarifa hizo zilikuwa zinagusia mwanamke ambaye polisi wanasema wamemkamata au ni mwanamke mwingine.

Malaysia kufikia sasa bado haijathibitisha rasmi iwapo mwanamume aliyeuawa ni Kim Jong-nam hasa, kwani alikuwa anasafiri akiwa anajiita Kim Chol.

Lakini serikali ya Korea Kusini imesema ina uhakika kwamba ndiye.

Idara ya ujasusi ya Korea Kusini imeambia wabunge kwamba inaamini Bw Kim aliuawa kwa kupewa sumu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kim Jong-nam alitumia muda wake mwingi nje ya Korea Kaskazini

Mauaji yake yakithibitishwa, basi kitakuwa kifo cha afisa wa juu zaidi anayehusishwa na Kim Jong-un tangu kuuawa kwa mjombake Chang Song-thaek, aliyeuawa kwa amri ya serikali2013.

Korea Kaskazini haijazungumzia kisa hicho, lakini maafisa wake kutoka ubalozi Malaysia walizuru hospitali ya Kuala Lumpur ambapo mwili wa Kim unahifadhiwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii