Kanda za video katika Facebook sasa kucheza na sauti

Unapopitia video katika mtandao wako sauti ya video hiyo itasikika moja kwa moja na kupotea unapopita video hiyo hatua inayozipatia uzima video hizo
Image caption Unapopitia video katika mtandao wako sauti ya video hiyo itasikika moja kwa moja na kupotea unapopita video hiyo hatua inayozipatia uzima video hizo

Ukuaji mkubwa wa kampuni ya facebook unatokana na kusambazwa kwa kanda za video katika mtandao wake na kwamba kampuni hiyo imewaelezea wawekezaji kwamba inataka kuimarisha ufanisi huo.

Facebook tayari imetangaza mipango kuanza kuimarisha hatua hiyo huku wakileta mabadiliko ambayo wateja wengi hawatayafurahikia.

Kanda za video zimekuwa zikicheza kwa kipindi cha muda mrefu katika mtandao wa facebook huku ongezeko la filamu zisizo na sauti likishuhudiwa baada ya wachapishaji kubaini kuwa wateja wengi watakuwa wakiangalia badala ya kusikiliza sauti za kazi yao.

Lakini kuanzia sasa na mwisho wa mwaka huu mtandao wa facebook utaweka sauti katika kanda zake za video mpango ambao kampuni hiyo imekuwa ikiujaribu miongoni mwa wateja wake kwa muda mfupi.

Kampuni hiyo imesema kuwa imefanikiwa kupata majibu mazuri kufikia sasa.

Unapopitia video katika mtandao wako sauti ya video hiyo itasikika moja kwa moja na kupotea unapopita video hiyo hatua inayozipatia uzima video hizo kampuni hiyo ilieleza katika chapisho lake la blogu.

Haki miliki ya picha facebook
Image caption Facebook

Wakati watu wanapotazama video katika simu zao, hutarajia kusikia sauti wakati sauti za kanda hizo zinapoongezwa.

Hatahivyo kwa wale wasiotaka video hizo kutosikika wakati wanaposafiri katika basi ,hawafai kuwa na shaka kwani video hizo hazitosikika watakapo zima sauti za simu zao.

Uchunguzi umebaini kwamba unapowapatia wateja kitu kipya mara nyingi hukipendelea.