Mchezaji wa Nigeria aihama klabu ya Arsenal

Asissat Oshoala akiichezea klabu ya Arsenal nchini Uingereza Haki miliki ya picha THE FA
Image caption Asissat Oshoala akiichezea klabu ya Arsenal nchini Uingereza

Mchezaji wa Nigeria anayesakata soka ya kulipwa katika klabu ya Arsenal nchini Uingereza upande wa akina dada Asisat Oshoala ameondoka katika klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Dalia Quanjian nchini China.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alishinda tuzo la BBC mwanasoka bora wa kike mwaka 2015 kabla ya kujiunga na Arsenal akitoka Liverpool.

Aliisaidia Arsenal kushinda taji la FA katika uwanja wa Wembley mwaka 2016 na hivi majuzi alipewa tuzo la mwanasoka bora wa kike mwaka huu.

Aliwahi kulichezea taifa lake katika kombe la dunia la mwaka 2015 nchini Canada.