Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam

Kim alishambuliwa alipokuwa anasubiri kuabiri ndege kuenda Haki miliki ya picha AP
Image caption Kim alishambuliwa alipokuwa anasubiri kuabiri ndege kuenda

Washukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia.

Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malaysia ambaye anakisiwa kuwa mpenzi wake wote walikamatwa leo Alhamisi.

Mwanamke mmoja maabye alikuwa na hati ya kusafiri ya Vietnam naye amekamatwa.

Kim alifariki siku ya Jumatatau kutokana na kile kinachaoimiw akuwa aliwekeka simu wakati akisubiri kuabiri ndeg mjini Kuala Lumpur.

Polisi wanasema kuwa wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wake Kim licha ya matokeo kutotangazwa

Haki miliki ya picha REX/Shutterstock
Image caption Picha hii ya CCTV imepeperushwa nchini Korea Kusini na Malaysian

Washukiwa hao wawili wa wamezuiwa rumande kwa siku saba.

Kuna uvumi unaoenea kuwa Korea Kaskazini ilihusika na mauaji hao.

Picha moja kutoka kwa kamera za usalama ambayo imepepeshwa nchini Korea Kusini na Malaysia, inaonyesha mwanamke mwenye fulana nyeupe yenye jina "LOL".

Inaaminiwa kuwa Kim alishambuliwa kwenye ukumbi wa kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege na wanawake wawili waliotumia aina fulani ya kemikali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kim Jong-nam na ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Leo Alhamisi Korea Kaskazini inasherehekea kile kinachotajwa kuwa miaka 75 ya kuzaliwa kwa Kim Jong-il, mareheu kiongozi wa zamani na baba wa Kim Jong-nam na Kim Jong-un.

Image caption Familia inayoongoza Korea Kaskazini