Je, vitamin D inaweza kumkinga mtu asiambukizwe na mafua?

Watu walio na mafua Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu walio na mafua

Ushapatwa na mafua ya pneumonia? basi si wewe peke yako, wewe ni miongoni mwa asilimia 70 ya watu waliougua mafua au pneumonia nchini Uingereza.

Lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa watu milioni 3 huenda wakapata kinga ya mafua ikiwa watatumia vidonge vya Vitamin D.

Hiyo ni mara mbili ya watu ambao hupata kinga ya mafua kwa kupata chanjo.

Wale waliofanya utafiti huo wanataka Vitamin D kuongezwa kwa chakula ili kila mmoja aweze kupata vitamin hiyo.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Aina mbali mbali za vidonge

Wataalamu pia wanawashauri watu kujaribu kuchukua hatua ambazo zitawakinga kutokana na mafua.

Mafua ni virusi ambavyo husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine, na njia kuu ya kuzuia ni kutowakaribia watu walio wagonjwa wanaokohoa.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mwangaza wa jua

Vitamin D wakati mwigine inafahamika kama "sunshine vitamin" kwa sababu mara nyingi hupatikana kutokana na jua .

Kutokana na hali ya hewa ilivyo nchini Uingereza watu hawapati vitamin hiyo kutoka kwa jua kati ya mwezi Oktoba na Machi.