Mwanamke wa miaka 64 ajifungua mapacha Uhispania

Kujifungua huko kulionyshwa katika kanda ya video ambayo ilichapishwa na hospitali hiyo.
Image caption Kujifungua huko kulionyshwa katika kanda ya video ambayo ilichapishwa na hospitali hiyo.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amefanikiwa kujifungua mapacha -mvulana na msichana katika eneo la Burgos, kaskazini mwa Uhispania.

Hospitali ya Recoletas iliwapokea watoto hao kupitia upasuaji ,ambapo hufanyika husuasan wakati wa visa kama hivyo.

Mwanamke huyo ambaye hakutajwa amefanyiwa matibabu ya uzazi nchini Marekani kulingana na vyombo vya habari vya Uhispania.

Hospitali hiyo imechapisha kanda ya video kuhusu upasuaji huo. Mwaka 2012 mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike ambaye baadaye alichukuliwa na kulewa na huduma za kijamii licha ya wasiwasi kuhusu hali yake.

Wafanyikazi wa kijamii wanasema kuwa msichana huyo alilewa akiwa pekee ,akiwa na mavazi mabaya mbali na uchafu wa eneo alilokuwa.

Hakuna uamuzi uliochukuliwa kufikia sasa kuhusu mama ya mtoto huyo.

Yeye na mamake wanadaiwa kuwa katika afya nzuri hospitalini. Mvulana huyo ana uzito wa kilo 2.4 huku msichana akiwa na uzito wa kilo 2.2.

Haki miliki ya picha kanda ya video ya hospitali ya Recoletas
Image caption Mmoja wa mapacha hayo alipigwa picha mara moja baada ya kuzaliwa

Mama huyo alijifungua bila matatizo yoyote. Katika siku za hivi karibuni, wanawake wengine wawili wa Uhispania wamejifungua watoto wenye afya.

Mnamo mwezi Aprili 2016 mwanamke mmoja wa Kiindi aliye na umri wa miaka 70 Dajlinder Kaur ,alijifungua mtoto mwenye afya katika jimbo la Haryana nchini India baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kizazi chake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii