Marekani yataka Urusi itimize ahadi zake

Marekani
Image caption Bendera ya Marekani na Urusi

Katika mkutano wao wa kwanza, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amemwambia mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, kwamba nchi mbili hizo zitafanya kazi pamoja, lakini Urusi inatakiwa kutimiza ahadi yake.

Amesema Washington inatarajia Urusi kuthamini ahadi yake ya kimataifa iliyoweka kuhusu Ukraine na kuhakikisha inadhamiria kupunguza vurugu zilizopo nchini Ukraine.

Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Marekani, James Mattis, katika makao makuu ya NATO yaliyopo Brussels, ameonyesha kutokuwa na uwezekano wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Urusi.

Bwana Mattis amesema ushirikiano wa kisiasa hauna neno, lakini Urusi sharti ijisafishe kabla Marekani na Nato havijafikiria kuwa na uhusiano wa karibu wa kijeshi.