Manchester United, AS Roma zashinda Europa Ligi

Ulaya Haki miliki ya picha Google
Image caption Manchester United katika furaha ya bao 3-0

Mashetani wekundu wa Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Saint-Etienne, mabao yote ya United yamefungwa na Zlatan Ibrahimovic.

As Roma wakicheza ugenini wameshinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Villarrea, Tottenham Hotspurn wamepoteza mchezo ugenini kwa kuchapwa kwa bao 1-0 na Kaa Gent.

AZ Alkmaar wamelala nyumbani kwa kufunga 4-1 na Lyon, wajerumani wa Borussia Moenchengladbach nao wamepoteza kwa Fiorentina kwa kufungwa bao 1-0.

Athletic Bilbao wameshinda nyumbani kwa 3 - 2 dhidi ya Apoel Nicosia, Celta Vigo wamechapwa na Shakhtar Donetsk kwa bao 1-0. Anderlecht wameshinda 2 - 0 dhidi ya Zenit St. Petersburg.

Paok Thessaloniki wameshindwa kutamba nyumbani kwa kufunga na Schalke kwa 3-0,

Matokeo mengine

  • Astra Giurgiu 2 - 2 Genk
  • Rostov 4 - 0 Sparta Prague
  • Ludogorets Razgrad 1 - 2 FC Koebenhavn
  • Olympiacos 0 - 0 Osmanlispor FK
  • Hapoel Beer Sheva 1 - 3 Besiktas
  • Legia Warszawa 0 - 0 Ajax

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii