Mkuu wa Samsung Lee Jae-yong akamatwa Korea Kusini

Lee Jae-yong Haki miliki ya picha EPA

Mrithi wa kampuni kubwa ya vifaa vya elektroniki Korea Kusini Samsung Lee Jae-Yong, amekamatwa katika sehemu ya uchunguzi kuhusu kesi ya kuondolewa madarakani rais wa taifa hilo Park Guen-Hye.

Viongozi wa mashtaka wanaweza kumzuilia kwa hadi siku 20 kabla ya kuamua kumfungulia rasmi mashtaka.

Miongoni mwa mengine, anatuhumiwa kuhusika katika ufisadi.

Msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka Lee Kyu-chul anasema Lee Jae-yong alilipa zaidi ya dola 35 milioni za Marekani kwa nyakfu zinazoungwa mkono na Choi Soon-sil, rafiki wa Rais Park Geun-hye.

Mwendesha mashtaka huyo anasema pesa hizo zilikusudiwa kuhakikishia uungwaji mkono wa mpango wa kuunganisha kampuni mbili zilizohusishwa na Samsung.

Bw Lee amekanusha tuhuma hizo.

Mwezi uliopita, Bw Lee, anayefahamika pia kama Jay Y Lee, alihojiwa kwa zaidi ya 20 na maafisa wa mashtaka mjini Seoul lakini maafisa wa mashtaka waliamua kutomkamata wakati huo.

Hata hivyo, alihojiwa kwa mara ya pili wiki hii.

Ijumaa, mahakama ilisema kwamba ilikuwa "imekubali kwamba ni muhimu kumkamata kutokana na mashtaka yaliyoongezwa na ushahidi mpya uliopatikana".

Kwa sasa ni naibu mwenyekiti wa Samsung Electronics, lakini tangu babake, Lee Kun-hee, alipopata mshtuko wa moyo mwaka 2014, amekuwa akitazamwa kama mkuu wa kampuni hiyo.

Kashfa hiyo inatishia kumtoa madarakani Bi Park ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi mwa muda Mahakama ya Juu inapoendelea kuchunguza tuhuma dhidi yake na mswada wa kumuondoa madarakani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kumeshuhudiwa maandamano dhidi ya Rais aliyesimamishwa kazi Park Geung-hye
Haki miliki ya picha AP
Image caption Bi Choi amekanusha tuhuma dhidi yake lakini akaomba radhi kwa "kusababisha mtafaruku"

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii