Pakistan: Watu 72 wafariki shambulio la Islamic State katika madhabahu

Karachi Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahudumu wa hospitali wakijiandaa kupokea majeruhi nje ya hospitali Karachi

Watu 72 wamefariki dunia kwenye shambulio katika madhabahu maarufu ya Wasufi kusini mwa Pakistan, polisi wamesema.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika katikati mwa waumini katika madhabahu ya Wasufi ya mtakatifu Lal Shahbaz Qalandar katika mji wa Sehwan, mkoa wa Sindh.

Waziri mkuu Nawaz Sharif amelaani shambulio hilo.

Wapiganaji wa Islamic State, Taliban nchini Pakistan na makundi mengine ya wanamgambo, wamekiri kuhusika.

Madhabahu hayo ni miongoni mwa yale ya kale zaidi na yanayotukuzwa sana na yalikuwa yamejaa watu Alhamisi, kwani siku hiyo huchukuliwa kuwa tukufu kwa Waislamu kufanya sala katika madhabahu hayo.

Walioshuhudia wanasema mshambuliaji alijilipua watu walipokuwa wakicheza dansi ya imani.

Vyombo vya habari zinasema alirusha guruneti nakisha akajilipua.

"Niliona miili imetapakaa kote. Niliiona miili ya wanawake na watoto," mwanamume mmoja aliwaambia wanahabari.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto ni miongoni mwa waliojeruhiwa
Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Madhabahu hayo ni miongoni mwa madhabahu matakatifu zaidi Pakistan
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mshambuliaji alijilipua watu waliokuwa wakicheza dansi takatifu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii