Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari yuko wapi?

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari yuko wapi?

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliondoka nchini mwake na kwenda London wiki tatu zilizopita na hadi sasa bado hajarejea nchini mwake.

Wiki moja iliyopita, aliliomba Bunge idhini ya kuendeleza kile alichosema ni “likizo ya kimatibabu”.

Taarifa kutoka kwa afisi yake inasema madaktari walimshauri kukaa muda zaidi kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kimatibabu.

Kabla ya kuondoka, alikabidhi masuala ya uongozi kwa makamu wake Profesa Yemi Osinbajo.

Msemaji wake Malam Garba Shehu amesisitiza kwamba yuko buheri wa afya na hajalazwa hospitalini.

Lakini hilo halijawazuia raia wa Nigeria kuwa na wasiwasi kuhusu hali yake.