Watu milioni tatu hatarini kutokana na njaa Somalia

Watu milioni tatu hatarini kutokana na njaa Somalia

Watu wapatao milioni tatu nchini Somalia wanakabiliwa na baa la njaa kufuatia ukame ambao umeiathiri vibaya nchi hiyo kwa muda sasa.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa hali itakuwa mbaya zaidi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kuwanusuru waathiriwa.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi alizuru eneo la Puntland nchini Somalia, na kuandaa taarifa hii.