Serikali ya Kenya kupeleleza simu za raia

Watumiaji wa simu Haki miliki ya picha Tom Spender
Image caption Watumiaji wa simu

Mamlaka nchini Kenya imeanzisha harakati ya kuzishurutisha kampuni za simu nchini kuruhusu vitengo vya kijasusi kudukua mawasiliano ya raia.

Mamlaka ya mawasiliano nchini humo CAK imewaandikia wahudumu wa simu ikitaka kuchunguza mitandao yao ,hatua itakayowapatia uwezo kudukua simu zinazopigwa, ujumbe mbali na shughuli za kifedha.

Mpango huo utasababisha wamiliki milioni 30 wa simu nchini humo kupoteza hali yao ya faragha pamoja na uaminifu.

Wahudumu hao wa simu ni Safaricom, Airtel na Orange.

Mamlaka hiyo inasema kuwa mpango huo ambao pia unalenga kupiga marufuku simu bandia unatarajiwa kuidhinishwa ifikiapo wiki ijayo.

Hatahivyo kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa mpango katika vyombo vya habari.