Vituo hivyo vinaaminika kuwasaidia wapenzi wa jinsia moja

Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja

Serikali ya Tanzania imesitisha huduma za msaada kwa vituo 40 vya matibabu vinavyodaiwa kuwasaidia wapenzi wa jinsia moja kulingana na chombo cha habari cha AP.

Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini humo na wanaopatikana na hatia hupigwa faini ya miaka 30 jela.

Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja, Kulingana na chombo cha habari cha AP kilichomnukuu waziri wa afya Ummi Mwalimu.

Waziri wa afya pia alitangaza kwamba serikali inaongeza takriban vituo 3000 vya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi nchini humo, imeongezea AP.

AP imeongezea mwezi Septemba kwamba serikali itasimamisha kwa muda huduma ya mipango ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi inayolenga wapenzi wa jinsia moja.