Adama Barrow kuidhinishwa rasmi Gambia

Rais wa Gambia Adama Barrow Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Gambia Adama Barrow

Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow, ataidhinishwa rasmi kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa masaa machache yajayo, kufuatia kuondoka kwa Yahya Jameh, mwezi mmoja uliopita.

Jameh alitawala miongo miwili.

Maelfu ya watu, kukiwemo viongozi kadhaa wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria hafula hiyo katika mji mkuu wa Banjul.

Rais Barrow aliapishwa kuwa rais mwezi uliopita katika ubalozi wa Gambia katika taifa jirani la Senegal kabla ya mtangulizi wake kukubali kung'atuka mamlakani.

Image caption Bango la Adama Barrow lawekwa tayariu kwa sherehe yake

Bwana Jammeh alikuwa amekataa kukubali kushindwa katika Uchaguzi wa Disemba na aliondoka nchini tu baada ya kushinikizwa kufanya hivyo na viongozi wa mataifa ya Magharibi mwa Afrika.