Suarez: Barcelona italipiza kisasi dhidi ya PSG

Suarez akikabwa na mchezaji wa PSG wakati timu yake ilipobebeshwa mabao 4-0 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez akikabwa na mchezaji wa PSG wakati timu yake ilipobebeshwa mabao 4-0

Barcelona imesema kuwa haijasalimu amri kufuzu katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na mshambuliaji Luis Suarez.

Mabingwa hao wa Uhispania walishindwa 4-0 na klabu ya Paris St- Germain katika awamu ya kwanza ya raundi ya muondoano siku ya Jumanne.

Wanawaalika PSG kwa awamu ya pili katika uwanja wa Nou Camp tarehe 8 mwezi Machi lakini hakuna timu iliofanikiwa kukomboa na kupata ushindi baada ya kufungwa mabao manne katika raundi ya muondoano.

''Iwapo tunataka kuweka historia katika klabu hii basi tutalazimika kubadilisha matokeo hayo alissema mshambuliaji huyo wa Uruguay.Sisi ndio timu bora duniani.Na iwapo kuna timu ambayo inaweza kubadili matokeo hay ni Barcelona''.

Barcelona imeshinda kombe la Ulaya ama lile la vilabu bingwa Ulaya mara tano na wamefanikiwa kufuzu katika robo fainali mara tisa mfululizo.

''Kushindwa tulivyoshindwa ni vigumu na uchungu.Itakuwa vigumu sana lakini changamoto nzuri sana'', aliongezea.

Alipoulizwa kuhusu kocha wa klabu hiyo Luis Enrique ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu,Suarez alisema ''sote tunapaswa kulaumiwa''.

''hatukucheza vyema na sote lazima tuchukue jukumu la kushindwa''.

Barcelona ambayo iko katika nafasi ya pili katika jedwali la ligi na pointi moja nyuma ya viongozi Real Madrid wanakabiliana na Legannes nyumbani siku ya Jumapili.