Adama Barrow aidhinishwa kuwa rais wa Gambia

Rais Adama Barrow aidhinishwa rasmi kama kiongozi wa Gambia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Adama Barrow aidhinishwa rasmi kama kiongozi wa Gambia

Adama Barrow ameidhinishwa rasmi kuwa rais wa taifa la Gambia .

Alikula kiapo mbele ya umati mkubwa wa watu uliojaa katika uwanja wa mji mkuu wa Banjul .

Mtangulizi wake Yahya Jammeh aliwachia mamlaka mnamo mwezi Januari baada ya kupoteza uchaguzi mbali na kutishiwa kwamba angeondolewa mamlakani kwa nguvu.

Rais aliyeng'atuliwa mamlakani na Jammeh miaka 23 iliopita Dawda Jawara ambaye ana umri wa miaka 92 alialikwa katika hafla hiyo.

Rais Barrow alikula kiapo kwa mara ya kwanza mwezi uliopita katika sherehe iliofanywa nchini Senegal akihofia maisha yake.