Jeshi la Iraq laanza kuishambulia IS mjini Mosul

Image caption Mwaandishi wa BBC Quentin Somerville, ambaye yuko pamoja na majeshi ya Iraq vitani, ametuma picha hii kutoka eneo hilo

Operesheni kali ya kuutwa tena eneo la magharibi mwa Mosul

Waziri mkuu wa Iraqi Haider al-Abadi ametangaza kuanza rasmi kwa operesheni kali ya kuutwa tena eneo la magharibi mwa Mosul, kutoka mikonini mwa wapiganaji wa Islamic State.

Hapo jana Jumamosi, jeshi la angani la Iraq lilirusha kutoka angani vijikaratasi nvyenye ujumbe wa kuwaonya raia dhidi ya hatari na uzito wa mapigano yanayotarajiwa.

Mosul ni mji wa mwisho mkubwa kwa maficho ya IS nchini Iraq.

Mwezi uliopita, serikali ya Iraq ilitwaa udhibiti wa sehemu ya mashariki mwa Mosul, katika mapigano makali yaliyodumu majuma kadhaa.

Umoja wa mataifa umeonya kuwa, kigezo cha kwanza ni kuwahakikisha usalama, mamia kwa maelfu ya raia waliokwama katika mji huo.

"Tunatangaza kuanza rasmi kwa mkondo mpya wa operesheni, tunakuja Nineveh kukomboa eneo la magharibi mwa Mosul," Bw Abadi alisema katika ujumbe wa moja kwa moja wa televisheni, huku akiashiria jimbo ambalo Mosul ni mji wake mkuu.

"Jeshi letu linaanza juhudi za kuwaokoa raia kutoka katika ukandamizaji wa Daesh [IS]," aliongeza, kama ilivyotangazwa na shirika la habari la AFP.

Kwa sasa jesjhi la Iraqi, limezingira eneo la magharibi mwa Mosul, huku jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani, limekuwa likitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya maeneo ya IS.