Korea Kaskazini ndiyo ilimuua Kim Jong-nam, yadai Korea Kusini

Kim Jong-nam Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kim Jong-nam

Korea Kusini inasema inaamini kuwa utawala wa Korea Kaskazini ndio ulihusika na kuuawa kwa Kim Jong-nam.

Ngugu huyo wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, aliuawa kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia wiki iliyopita.

"Tunaamini utawala wa Korea Kaskazini ndio ulihusika na kisa hii kwa sababu washukuwa watano ni raia wa Korea Kaskazini," alisema msemaji wa wizara ya upatanishi ya Korea Kusini.

Idara ya Polisi nchini malaysia inasema kuwa inawatafuta zaidi ya washukiwa wanne kutoka Korea Kaskazini kuhusiana na mauaji ya kakake wa kambo, Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Kim Jong-nam, alifariki muda mfupi baada ya kupuliziwa sumu katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpur, juma lililopita.

Polisi wamewatambua washukiwa wanne wote wanaume wenye umri kati ya miaka 43 hadi 47, ambao wanasemekana tayari wameondoa Malaysia.

Watu wanne wanazuiliwa korokoroni kuhusiana na mauaji ya Kim, akiwemo mwanamke ambaye anasemekana kuwa alihadaiwa kutekeleza mauaji hayo.

Polisi wanajaribu kuwatafuta jamaa ya mhasiriwa ili kusaidia katika uchunguzi.

Marehemu Kim Jong-nam, alitarajiwa kutawala Korea Kaskazini, lakini walikosana na babake marehemu Kim Jong-il lakini akaamua kukimbilia uhamishoni.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kim Jong-nam na ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un