Mwanaharakati anayeshukiwa kupewa sumu Urusi apelekwa matibabu ng'ambo

Bwana Kara-Murza (kushoto) alikuwa mshirika wa karibu kwa kiongozi wa upinzani aliyeuawa Boris Nemtsov (kulia) Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bwana Kara-Murza (kushoto) alikuwa mshirika wa karibu kwa kiongozi wa upinzani aliyeuawa Boris Nemtsov (kulia)

Mwana harakati wa Urusi, Vladimir Kara Murza, ameondoka nchini baada ya kulazwa hospitali kwa zaidi ya majuma mawili, akiwa mahututi.

Inashukiwa kuwa mwana harakati huyo alipewa sumu.

Karatasi za hospitali zinasema aliugua kutokana na kitu kisichojulikana.

Alisafirishwa kwa ndege kutoka Urusi, akifuatana na mkewe na tabibu, kuenda kuendelea kutibiwa nchi za nje.

Taarifa ilisema kuwa Bwana Kara Murza, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa, Boris Nemtsov, anakusudia kuendelea na kazi yake ya kurejesha demokrasi nchini Urusi.