Mzozo waibuka kati ya Korea Kaskazini na Malaysia kufuatia kuuawa kwa Kim Jong-nam

Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia

Malaysia imechukua hatua za kidimpaoa sdhid ya Korea Kaskania kuafuatyai kuuwa kwa Kim Jon-nam ndugu wa kambo wa kiongzia wa akorea Kaskaziania Kim Jon-un.

Kim alifariki kwa njia ya kutatanisha wiki iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Polisi wanaamini kuwa alipewa sumu.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia Kang Chol, anasema kuwa haamini uchunguzi wa Malaysia.

Malaysia imemuita balozi wake kutoka mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang, na kumuita balozi wa Korea Kaskazini wakitaka maelezo.

Polisi nchini malaysia kwa sasa wanasema kuwa wanawatafuta watu wanne raia wa Korea Kaskazini.

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia Kang Chol, anasema kuwa haamini uchunguzi wa Malaysia.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwanamume mmoja raia wa Korea Kaskazini tayari amekamatwa

Waziri mkuu nchi Malaysia ametetea polisi wa nchi hiyo na kusema kuwa anataka Korea Kaskazini kuelewa kuwa sheria inatumika nchini Malaysia.

Kanda moja ya video ambayo inaonyesha picha za CCTV za shambulizi dhidi ya Kim Jong-nam, imetokea na kupeperushwa na televisheni moja ya Japan.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Hong Song Hac, 34, na Ri Ji Hyon, 33, wanatafutwa na polisi wa Malaysia