Mashua ya kifahari ya mfanyabiashara wa Urusi yakamatwa Gibraltar

Mashua iliyokamatwa kwa jina Yacht A

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mashua iliyokamatwa kwa jina Yacht A

Gibraltar imekamata mashua moja ya kifahari inayomilikiwa na tajiri raia wa Urusi, ambayo inatajwa kuwa moja ya mashua za kifahari kubwa zaidi duniani.

Hii ni baada ya kampuni moja ya Ujerumani iliyoijenga mashua hiyo, kudai kuwa mmiliki ana deni lake la dola milioni 16.3.

Madai hayo yamesababisha mashua hiyo ya Andrey Melnichenko kuzuiliwa katika kisiwa cha Gibraltar, ambayo ni koloni ya Uingereza tangu siku ya Jumatano.

Chombo hicho chenye usajili wa Bermuda kilichojengwa na kampuni ya Nobiskrug, kiliondoka kaskazini mwa Ujerumani wiki mbili zilizopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

The wealthy Russian also owns Motor Yacht A - seen here next to HMS Belfast on the Thames

Mashua hiyo ni ya urefu wa umbali wa mita 143 na urefu wa mita 100 kuenda juu

Inaripotiwa kugharimu Euro milioni 400 kujengwa.

Kulingana na jarida na Forbes mmiliki wa mashua hiyo Andrey Melnichenko ambaye anamiliki biashara kadha zikiwemo za mbolea, makaa ya mawe, na vya nishati ana utajiri wa dola bilioni 13.2.

Pia anamilliki mashua nyingine ya kifahari inayoitwa Motor Yacht A, ambayo inaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kuuzwa baada ya kuzinduliwa mwaka 2008.