Upinde nadra wa mvua wasisimua Singapore

Picha ya upinde wa mvua Singapore 20 Februari 2017

Chanzo cha picha, Fazidah Mokhtar

Tukio nadra sana angani, la kutokea kwa upinde unaofanana na ndimi za moto, lilitokea katika anga la Singapore na kuwasisimua sana wakazi.

Upinde huo ulidumu kwa takriban dakika 15 na ulionekana kote katika kisiwa hicho.

Taarifa za habari zinaashiria kwamba huenda ulitokana na miali ya jua kuchepuzwa au kupindishwa na chembechembe za barafu kwenye mawingu.

Wengine wanasema huenda ilitokana na kutawanyishwa kwa miali ya jua na matone ya maji angani.

Chanzo cha picha, Nayla Yg Tercakiti

Fazidah Mokhtar, anayefanya kazi katika kituo kimoja cha kuwahudumia watoto, aliambia BBC kwamba alianza kuuona upinde huyo mwendo wa saa kumi na moja na dakika kumi jioni Jumatatu.

"Ulianza kama mdua mdogo wa rangi ya machungwa kisha ukawa mkubwa na mkubwa hadi marangi yote ya upinde yakaonekana. Ulidumu kwa dakika 15 hivi kisha ukaanza kufifia pole pole na kisha kutoweka."

Alisema "watoto shuleni, baadhi ya wazazi, na wafanyakazi pia, walifurahia sana upinde huo na kusema ni tukio la kupendeza sana."

Chanzo cha picha, Zhou Guang Ping

Chanzo cha picha, Zhou Guang Ping

Chanzo cha picha, Benjamin Kong

Chanzo cha picha, @HamsLuminiq