Kim Jong-nam: Ulinzi mkali hospitalini unakohifadhiwa mwili

Kuala Lumpur (21 Feb 2017)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Polisi wa Malaysia wakishika doria nje ya hospitali unakohifadhiwa mwili wa Kim Jong-nam

Maafisa wa serikali ya Malaysia wamesema bado hawajabaini nini kilisababisha kifo cha ndugu wa rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Mkurugenzi mkuu wa afya Noor Hisham Abdullah amewaambia wanahabari kwamba hawajapata ushahidi wowote wa kutokea kwa mshtuko wa moyo au vidonda vilivyotokana na kudungwa mwilini.

Amesema uchunguzi kwenye maabara pia haukuweza kuutambia mwili huo.

Kim Jong-nam anadaiwa kuwa mwanamume aliyefariki wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, baada ya kuonekana kana kwamba alipewa sumu.

Pyongyang imetilia shaka utambulisho wa mwili huo na imeitaka Malaysia kusalimisha mwili huo kwa maafisa wa Korea Kaskazini.

Jumatatu, Malaysia ilimuita nyumbani balozi wake kutoka Korea Kaskazini huku mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kutanda.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia

Maafisa wa Malaysia wamesema wanahitaji kupata vinasaba kutoka kwa jamaa za Kim Jong-nam ndipo waweze kuutambua mwili huo kikamilifu.

Ulinzi mkali umewekwa katika hospitali ambapo mwili huo unahifadhiwa.

Kuna taarifa kwamba huenda mwanawe Kim Jong-nam, Kim Han-sol, amesafiri Malaysia kuuchukua mwili huo. claim the body.

Jumanne, maafisa wa polisi waliokuwa na silaha kali walifika katika hospitali hiyo ya Kuala Lumpur, na baadaye wakafuatwa na maafisa wa usalama waliokuwa katika magari yasiyokuwa na utambulisho rasmi.

Mwanawe Kim, Kim Han-sol amekuwa akiishi Macau.

Chanzo cha picha, REX/Shutterstock

Maelezo ya picha,

Mwanamke mmoja alikamatwa kuhusiana na mauaji hayo, na alisema alidhani ulikuwa mchezo wa kuigiza

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Raia wanne wa Korea Kaskazini wanasakwa na wachunguzi wa jinai kuhusiana na kifo cha Kim