Wanaume bado wanahitaji elimu ya Ukeketaji nchini Tanzania

Katika baadhi ya nchi za Afrika,Ukeketaji ni hatua ya kutekeleza masuala ya mila na desturi zao, japo hatua hiyo inapingwa kutokana na madhara yake.Nchini Tanzania jamii ya wakurya mkoani Mara Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo, inakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wanawake na wasichana hulazimishwa kukeketwa,Jambo ambalo limewafanya baadhi ya wasichana kutoroka na kwenda kujihifadhi katika vituo vya misaada ili kuepuka kukeketwa.

Mwandishi wa BBC Munira Hussein amesafiri na kufika kwenye jamii hiyo ya Wakurya na kujionea hali ilivyo.