Muhammadu Buhari kukaa muda zaidi Uingereza

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Serikali ya Nigeria, imejaribu kuwahakikishia raia nchini humo kuhusiana na afya ya rais Muhammadu Buhari, mwezi mmoja baada yake kuelekea Uingereza kwa matibabu.
Hapo awali alitazamiwia kufanyiwa matibabu kwa wiki mbili lakini kufikia sasa bado hajarejea nchini mwake
Serikali hiyo imesema kupitia taarifa kwamba hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi, ikiongeza kwamba uchunguzi aliofanyiwa Rais Buhari, ambao amekuwa akifanyiwa, kila mwaka umebaini rais huyo anahitaji muda zaidi wa mapumziko
Viongozi hao hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana na afya ya Bw Buhari, na kumekuwa na wasiwasi mwingi hasa katika vyombo vya habari nchini Nigeria na mitandaoni.
Msemaji wa bw Buhari Garba Shehu ameweka taarifa hiyo kwenye mtandao wake wa Facebook.