Gabon yapoteza asilimia 80 ya ndovu wake

Gabon inaamiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya ndovu wa msituni waliosalia.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Gabon inaamiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya ndovu wa msituni waliosalia.

Ripoti mpya inasema kuwa Gabon imepoteza asilimia 80 ya ndovu wake kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita

Watafiti wanasema kuwa ndovu wanauawa kwa pembe zao na wawindaji ambao huingia nchini kutoka nchi jirani ya Cameroon.

Gabon inaamiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya ndovu wa msituni waliosalia.

Lakini watafiti kutoka chuo cha Duke nchini Marekani wanasema kuwa ndovu 25,000 wamuawa kwenye mbuga ya Minkebe eneo ambalo limekuwa likichukuliwa kama hifadhi.