Tumbili 57 wauawa kwa kuwa na jeni tofauti Japan

Tumbili wa barafu wa Japan
Maelezo ya picha,

Tumbili wa barafu wa Japan

Hifadhi moja wa wanyama ambayo ni ya kuwahifadhi tumbili wa barafu imewaua tumbili 57, ambao ilikuwa ikiwahifadhi baada ya kugundua kuwa nyani hao walikuwa na maumbile ya kijenetiki ya familia tofauti .

Hifadhi hiyo ya Takagoyama ilichukua hatua hizo baada ya uchunguzi wa DAN kuonyesha kuwa theluthi moja ya tumbili walikuwa na jenetiki ya familia nyingine ambayo haitambuliwi kuwa ya asilia nchini Japan.

Afisa mmoja alisema kuwa tumbili hao walikuwa ili kulinda familia za asili.

Nyani hao waliuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu na msimamizi wa hifadhi akawaandaa maombi kwenye hekalu lililokuwa karibu.