Miili ya wahamiaji 74 yasombwa hadi fukwe za Libya

Miili ya wahamiaji 74 yasombwa hadi fukwe za Libya

Chanzo cha picha, IFRC MENA

Maelezo ya picha,

Miili ya wahamiaji 74 yasombwa hadi fukwe za Libya

Shirika la hilali nyekundu nchini Libya linasema kuwa limepata miili ya wahamiaji 74, ambayo ilisombwa hadi fukwe zilizo karibu na mji wa magharibi wa Zawiya.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, lilisema kuwa wahamiaji hao walikuwa kwenye mashua ambayo iliondoka nchini Libya siku ya Jumamosi ikiwa na watu 110.

Maiti hizo zitazikwa mjini Tripoli kwenye makaburi ya watu wasiotambuliwa.

Hivi majuzi Muungano wa Ulaya ulikubali kutoa msaada wa dola milioni 215 kwa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kupunguza idadi ya wahamiaji.

Mwaka uliopita wahamiaji 5000 walizama maji walipojaribu kufika ulaya wakipitia bahari ya Mediterranean.