Maduka ya wahamiaji yaporwa Afrika Kusini

Wahamiaji wa Afrika na kutoka Asia hukumbwa na ghasia nchini Afrika Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wahamiaji wa Afrika na kutoka Asia hukumbwa na ghasia nchini Afrika Kusini

Zaidi ya maduka 30 yanayomilikiwa na raia wa kigeni yameporwa sehemu mbili tofauti kwenye mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria.

Uporaji huo ulianzia eneo la Atteridgeville na kusambaa hadi eneo lililokaribu la Lotus Gardens. Hata hivyo polisi walifanikiwa kutuliza hali.

Baadhi ya wenye maduka walikuwa ndani lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Uporaji huo unatokea kabla ya maandamano yanayopangwa kufanyika siku ya Ijumaa na kundi dogo la Mamelodi Concerned Residents, kulalamikia wahamiaji wasiosajiliwa nchini Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wahamiaji wa Afrika na kutoka Asia hukumbwa na ghasia nchini Afrika Kusini

Mkutano wa makasisi wa kanisa katoliki wa nchi za kusini mwa Afrika, umeitaka serikali kudhibiti mipaka. Pia makasisi hao wametaka mashirika ya usalama kutambua ghasia kabla hazijalipuka.

Afrika ina ukosefu wa ajira wa asilimia 25 sababu ambayo imesababisha wageni kulengwa tangu umalizike ubaguzi wa rangi mwaka 1994.