Unawezaje kumaliza tatizo la hewa chafu unakoishi?

Hong Kong China

Chanzo cha picha, Lam Yik Fei/Getty

Maelezo ya picha,

Mji wa Hong Kong

Shirika la Afya Duniani linakadiria kwamba watu 9 kati ya watu 10 hupumua hewa chafu duniani.

Kuanzia Machi 6-12, BBC itakuwa ikiangazia njia mbalimbali za kupunguza uchafuzi wa hewa.

Suluhu mbalimbali, kuanzia kwa biashara na teknolojia hadi sheria zinazoweza kupitishwa na mabadiliko ya tabia, zitaangaziwa.

Wiki hiyo yote, kutakuwa na taarifa za kipekee, zikiangazia mifano ya juhudi ambazo zimefanikiwa pamoja na mazungumzo na watu kama wewe kuhusu suala hili.

Tunataka WEWE ushiriki katika mradi huu.

Iwapo ungependa kushiriki, basi tuambie ungependa nini kibadilishwe ili kupunguza uchafuzi wa hewa. Andika mambo ambayo ungependa yabadilishwe kwenye karatasi kubwa na ujipige picha ukiwa umeishika karatasi hiyo.

Anza pendekezo lako la suluhu kwa "Ningependa - ongeza suluhu hapa - kupunguza #UchafuziWaHewa - andika mji au jiji lako hapa - #NiwezeKupumua".

Hapa ni mfano, kwa Kiingereza, kutoka kwa Adelaide Arthur mjini Accra, Ghana kukusaidia kukuongoza:

Chanzo cha picha, Adelaide Arthur

#NiwezeKupumua si kampeni. Tunataka usambaze picha na mapendekezo ambayo yanaweza kuwahamasisha wengine kutoa mapendekezo yao ya njia ambazo wanadhani zinaweza kutumiwa kupunguza uchafuzi wa hewa.

Unaweza kututumia picha zako kwa:

Kutumia barua pepe yourpics@bbc.co.uk

Kutuma kama ujumbe wa simu kwa 61124 au +44 7624 800 100 iwapo unaishi nje ya Uingereza

Au WhatsApp kwa +254 712 640 787

Au kuzipakia kwa kutumia fomu hii

Au kupitia Twitter katika @bbcswahili

Unaweza pia kuandika kwenye mitandao yako ya kijamii na utumie kitambulisha mada #NiwezeKupumua

Chanzo cha picha, Joab Frank Chakhaza