Wameanza kujisajili katika sajili za wapiga kura.

Wafungwa nchini Kenya wakijisajili katika sajili za wapiga kura
Maelezo ya picha,

Wafungwa nchini Kenya wakijisajili katika sajili za wapiga kura

Wafungwa nchini Kenya wameanza kujiandikisha kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.

Ifikiapo mwezi Agosti Wakenya hao wanaohudumia vifungo vyao katika magereza mbalimbali watashiriki katika zoezi hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo.

Hatahivyo wafungwa hao watashiriki katika uchaguzi wa rais na sio wabunge ama wawakilishi wengine wowote.

Jamaa walikubaliwa kupiga kura mara moja tu wakati wa kura ya maoni 2010 wakati ambapo wakenya walikuwa wanapiga kura ya kubadilisha katiba.

Maelezo ya picha,

Ronald Mwachie amesajiliwa na atashiriki katika uchaguzi huo kwa mara ya kwanza

Kulingana na tume ya uchaguzi ,Kenya ina takriban jela 118 zinazobeba wafungwa 49,000 lakini ni wafungwa 10,000 walio na vitambulisho ambavyo hutumika wakati mtu anaposajiliwa kushirika katika shughuli hiyo.

Wengi walijisajili. Ronald Mwachie ambaye amehudumia miaka 20 katika kifungo cha maisha amesema kuwa atashiriki katika uchaguzi huo kwa mara yake ya kwanza.