Wahamiaji wanaoingia Uingereza waongezewa masharti

Waingereza wanaotaka kuoa nje ya taifa wawekewa masharti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waingereza wanaotaka kuoa nje ya taifa wawekewa masharti

Mahakama ya juu zaidi nchini Uingereza imeamua kuwa serikali ina haki ya kuweka kiwango cha chini zaidi cha mshahara ambacho mwanamke au mwanamme anapaswa kupokea ili aruhusiwe kumwingiza mchumba wake nchini humo.

Sheria iliyobuniwa miaka mitano iliyopita ina walazimu wanaume au wanawake kupokea mshahara wa zaidi ya dola elfu ishirini na tatu, kabla ya kukubaliwa kuwaalika wachumba wao ambao ni raia wa kigeni.

Hata hivyo sheria hiyo haiwahusu raia wengi wa mataifa ya Ulaya.

Majaji wamesema kuwa sheria hizo zilikuwa na malengo ya kisheria ingawa haiwajali watoto wanaohusika katika ndoa za aina hiyo.

Lord Carnwath,mmoja wa majaji waliotoa hukumu hiyo amesema sheria juu ya kipato cha chini inalenga kuhakikisha wanandoa hashawishiwi na mkumbo wa kukimbilia faida ya ustawi na kuwa na rasilimali za kutosha kugharamia maisha yao nchini Uingereza.

Kwa upande wake Saira Grant,amesema familia za raia wa Uingereza zinavunjwa kwa sababu ya kizuizi kilichobuniwa na binadamu.