Marekani: Wanasiasa ndio wamesababisha njaa Sudan Kusini

Takiban watu milioni 5.5 nchini Sudan Kusini wanakumbwa na hatari ya hali mbaya ya njaa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Takiban watu milioni 5.5 nchini Sudan Kusini wanakumbwa na hatari ya hali mbaya ya njaa.

Marekani inasema kuwa njaa iliyotangazwa maeneo ya Sudan Kusini imesababishwa na wanasiasa ambapo imewalaumu viongozi wa nchi hiyo.

Takiban watu milioni 5.5 nchini Sudan Kusini wanakumbwa na hatari ya hali mbaya ya njaa.

"Haya ni matokeo ya moja kwa moja ambayo yamesababishwa na mzozo wa muda mrefu kutoka kwa vingozi wa Sudan Kusini, ambao hawataki kuweka kando maslahi yao ya kisiasa kwa manufaa wa watu wao." Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani amesema.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Papa Francis anataka watu wa Sudan Kusini kupelekewa chakula

Kwa upande wake kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis, ametaka msaada kutumwa kwa mamilioni ya watu wanaokumbwa na njaa Sudan Kusini.

Akiongea mjini Vatican Papa Francis alisema kuwa ni wakati wa kujitolea zaidi, sio kwa kuongea tu bali kwa kutoa chakula na kukiruhusu kuwafikia watu wanaotaabika.

Sudan Kusini imekumbwa na vita tangu mwaka 2013, ambapo zaidi ya watu milioni 3 wamelazimika kukimbia makwao.