Facebook imefanya hivyo kutoa adhabu.

Watoto waliyodaiwa kuugua saratani

Chanzo cha picha, FACEBOOK/MERCURYPRESS

Maelezo ya picha,

Watoto waliyodaiwa kuugua saratani

Facebook imefanikiwa kufunga ukurasa uliyokuwa umechapisha picha za watoto waliyodaiwa kuugua saratani.

Hii ni mara ya pili mtandao huo wa kijamii umefunga akaunti ya mteja wake kufatia malalamishi na baadaye kuifungua tena baada ya saa chache.

Msemaji wa facebook hata hivyo hakuweza kuelezea hatua hiyo na kuongeza kuwa suala hilo bado linachunguzwa. Mmoja wa wataalamu wa wa mambo ya interneti

amedhihaki hatua hiyo na kutilia shaka mfumo wa facebook wa kushughulikia malalamishi. Siku ya jumanne BBC iliripoti kisa cha mtoto kutoka Cambridgeshire

Chanzo cha picha, FACEBOOK/MERCURYPRESS

Maelezo ya picha,

Mmoja wa watoto waliyodai wanaugua saratani

ambaye picha yake ilitumiwa kutoa ombi la uongo la kutaka msaada. "Huyu mtoto mdogo anaugua saratani na anahitaji pesa kwa ajili ya upasuaji." Tangazo hilo liliongeza

kuwa facebook itatoa kama msaada fedha ambazo itakusanya kutoka kwa ada itakayotoza kwa yule atakaye bonyeza "like" kutoa maoni au kusambaza ujumbe huo. Watu zaidi

ya milioni moja waliitikia mwito huo. Picha hiyo ilitumwa mtandaoni mwanzo wa mwezi Februari.

Chanzo cha picha, FACEBOOK

Maelezo ya picha,

Ukurasa huu ulikuwa umefungwa lakini ukachapishwa tena Jumanne

Wataalamu wa masuala ya usalama wamesema mbinu kama hizo hutumiwa sana na walaghai na wanajaribu sana kuwahusisha watu wengi kadri ya uwezo wao na baadaye

huwafuatilizia kwa ujumbe,kutengeneza faida kupitia tangazo hilo au kuwauzia wafanyibiashara wasiyokuwa na habari mawasiliano hayo. Mamake mtoto huyo Sarah Allen kutoka St Neots,Cambridgeshire,ameilezea BBC jinsi alivyohuzunishwa na tukio hilo.