Kijiji kinachohama mita moja kila siku nchini Italia

Kijiji kinachohama mita moja kila siku nchini Italia

Wakazi wa nyumba 33 wamehamishwa makwao na wengine 100 wakaachwa bila makao kutokana na maporomoko ya ardhi ambayo yanaathiri kijiji cha Ponzano nchini Italia.

Maafisa wanasema mlima kwenye kijiji hicho umegawika mara mbili na kipande kimoja cha ardhi kinasonga kwa kasi ya mita moja kwa siku.

Kijiji hicho kinapatikana katika eneo la Abruzzo ambalo liliathiriwa na mitetemeko ya ardhi mwaka 2016.