Farmajo apendekeza Hassan Kheyre awe waziri mkuu Somalia

Mohamed Abdullahi Farmajo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mohamed Abdullahi Farmajo

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amependekeza uteuzi wa Hassan Ali Kheyre kuwa waziri mkuu mpya wa Somalia.

Bw Kheyre hajahusika sana na siasa za Somalia.

Aliwahi kuhudumu kama mkuu wa shirika linaloangazia masuala ya wahamiaji la Norwegian Refugee Council [NRC] nchini Norway.

Amekuwa akihudumu kama mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya Soma Oil & Gas in East Africa, yenye makao makuu yake nchini Uingereza.

Bw Kheyre ana uraia wa mataifa mawili, Somalia na Norway.

Bw Farmajo amependekeza uteuzi wa Kheyre siku moja baada ya kuapishwa rasmi kuongoza taifa hilo katika sherehe iliyohudhuria na viongozi wa nchi jirani Hassan akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Akiidhinishwa na Bunge, Bw Kheyre atachukua nafasi ya Omar Abdirashid Ali Sharmarke ambaye alihudumu kama waziri mkuu kuanzia 2014.