Wazee wasimulia madhila katika vituo vya kuwatunza Tanzania

Wazee wasimulia madhila katika vituo vya kuwatunza Tanzania

Uzee ni umri ambao mtu huhitaji uangalizi wa karibu katika kila jambo.

Idadi ya wazee nchini Tanzania inakadiriwa kuongezeka ambapo utafiti unaonyesha ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na wazee wengi zaidi watakaohitaji kutunzwa katika vituo.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amesafiri hadi Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Kusini magharibi mwa Tanzania akatembelea kituo cha wazee na kutuandalia taarifa ifuatayo.