Simu ya Buhari yaondoa wasiwasi Nigeria

Rais Muhammadu Buhari akipiga simu

Chanzo cha picha, Red Media Africa

Maelezo ya picha,

Rais Muhammadu Buhari akipiga simu

Rais wa Nigeria hatimaye amepiga simu nchini humo na kuelezea kuwa yu buheri wa afya.

Mazungumzo hayo kati ya gavana wa jimbo la Kano Abdullahi Umar ganduje yalichezwa katika kipaza sauti katika mkutano wa mamombi ili raia wasikie.Baadaye yalichezwa katika vituo vya redio.

Kwa wafuasi wake waliokuwa na wasiwasi simu hiyo ilifutilia mbali uvumi kuhusu kifo chake.

Wengine wamekuwa wakisema kwamba Buhari mwenye umri wa miaka 74 alikuwa mgonjwa kupitia kiasi ama hakuweza kuzungumza lakini simu hiyo ilionyesha kwamba yuko hai na kwamba anapumzika.

Ripoti za vyombo vya habari nchini Nigeria zinasema kuwa watu katika mkutano huo wa maombi walibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kusikia sauti ya Buhari, lakini waandishi wanasema kuwa hiyo sio sababu na kwamba walikuwa wakimsifu mola kwa sauti ya juu na kumuombea Buhari.

Haya hapa mazungumzo hayo:

Gavana wa Kano :Hali yako ya kiafya?

Rais Buhari: Mungu asifiwe nasikia vizuri

Umma: Mungu ni mkubwa {kwa sauti kubwa}

Gavana wa Kano: Wanakusikia ukijibu maswali yangu.

Rais Buhari: Wapatie salamu zangu.

Gavana wa Kano :Siku ya ijumaa misikiti yoye itakuombea mungu tena.

Rais Buhari: Sifa zote zimuendee Mungu.Mungu azikubali dua zenu.

Umma: Mungu ni mkubwa {kwa sauti ya juu}