Chris Brown akatazwa 'kumuona' mpenziwe wa zamani

Chris Brown na mpenziwe wa zamani Karrueche Tran
Maelezo ya picha,

Chris Brown na mpenziwe wa zamani Karrueche Tran

Chris Brown amekatazwa kumuona mpenziwe wa zamani baada ya kudai kwamba alitishia kumuua mwezi Disemba.

Karrueche Tran amepewa agizi hilo dhidi ya msanii huyo na mahakama akisema amemtishia kupitia jumbe tangu mwezi Disemba.

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 28 amemshutumu mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kumpiga tumboni na kumsukuma kwenye ngazi nyumbani lakini anasema kuwa hakuripoti kwa polisi.

Wawili hao walikuwa wapenzi 2015 lakini wakawachana baada ya miezi kadhaa.

Nakala za mahakama zilisema: Aliambia watu kadhaa kwamba angeniua.Amesema kuwa iwapo hakuna mtu atamuua basi ataniua.Nina jumbe kutoka Disemba 2016 hadi Januari 2017 ambapo amenitishia ikiwemo kunipiga na kuniharibia maisha.