Mbinu mpya ya upasuaji yazinduliwa Tanzania

Nchini Tanzania, watoto waliozaliwa na mapungufu mbalimbali kama vile kutokuwa na sehemu ya haja kubwa, na kokwa kwenye korodani, wataweza kufanyiwa upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic Surgery).

Hii ni baada ya Madaktari bingwa kutoka nchini Saudia wakishirikiana na wenzao katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kuanzisha huduma hiyo, baada ya kufanya upasuaji huo kwa mara ya kwanza kwa watoto nchini.

Halima Nyanza anaarifu zaidi