Wanajeshi Guatemala kuzuia kuavya mimba

Wanajeshi wa Guatemala wazuia kuavya mimba
Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Guatemala wazuia kuavya mimba

Jeshi la nchini Guatemala limesema litapiga marufuku shughuli za kutoa mimba zinazofanywa na kundi la madaktari wa kigeni na wauguzi wanaowasili nchini humo kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji mimba bure kwa wanawake wakiwa na mimba changa.

Shirika hilo lenye makazi yake nchini Uholanzi liitwalo Women on Waves,lilijitolea kuwachukua wanawake wajawazito kwa boti mpaka kwenye eneo la kimataifa la bahari, ambapo zoezi hilo hufanyika bila kuvunja sheria za nchi hiyo.

Utoaji mimba huruhusiwa pale ambapo maisha ya mama yako hatarini

Boti hiyo iliwasili kwenye pwani ya bahari ya Pacific sikuya jumatano lakini huenda wakalazimika kuondoka haraka.

Wataalam hao wamesema vitendo vya utoaji mimba kiholela huhatarisha maisha ya zaidi ya wanawake 60,000 wa Guatemala kila mwaka.