Wakazi wa Sumbawanga wasimulia kuhusu tetemeko Tanzania

Tetemeko la ardhi lilikumba maeneo ya Ziwa Tanganyika usiku wa kuamkia leo na kutikisa maeneo mengi kaskazini mwa Zambia, magharibi mwa Tanzania na pia baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kuwepo kwa majeruhi kufuatia tetemeko hilo lililokuwa na nguvu ya 5.7.

Mashuhuda wa tukio hilo walioko Magharibi mwa Tanzania wameiambia BBC kwamba mtikisiko huo ulisababisha taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa Rukwa.